Inapakia...
Inapakia...


✦ Maarifa, Imani, Huduma ✦
MUUNGANIKO WA MAARIFA NA IMANI
Tunachapisha na kukuza maarifa ya kisayansi yanayofikika, yaliyojengwa juu ya maadili—tukiunga mkono afya, elimu na ustahimilivu wa jamii.
📍 Sokoine University of Agriculture, Morogoro
Gundua muunganiko wa busara kati ya sayansi na dini kwa safari ya maarifa, tafakuri, na huduma.
Uchunguzi wa fizikia, biolojia, na teknolojia unaoonyesha umahiri wa Muumba katika uumbaji.
Maswali ya maisha, kusudi, na maana ya ukweli kupitia imani yenye tafakuri ya kina.
Uchunguzi wa asili ya ulimwengu, mifumo ya nyota, na nafasi ya mwanadamu katika historia ya uumbaji.
Maajabu ya DNA, seli, na usanifu wa maisha katika viwango vya kemia na molekuli.
Majadiliano ya maadili kuhusu matumizi ya teknolojia na wajibu wa maarifa kwa jamii.
Kusherehekea uzuri wa asili kutoka kwa chembe ndogo hadi kwa galaksi kubwa.

Tangu
SUA, Morogoro
Tunachapisha na kukuza maarifa ya kisayansi yanayofikika, yaliyojengwa juu ya maadili—tukiunga mkono afya, elimu na ustahimilivu wa jamii.
Tunaunganisha maarifa, imani na huduma
Injili ya sayansi imejikita kutoa masomo mbalimbali kivitendo kuhusiana na Elimu ya kweli na Malezi. Katika Kitengo cha Elimu na Malezi; Injili ya sayansi inashirikiana na wasomi mbalimbali wenye motisha ya kusaidia jamii zao kwa kutoa Elimu bora nje na mfumo tegemezi wa elimu. Malengo ya injili ya sayansi ni kutengeneza kizazi ambacho kitakuwa na Elimu ya kujitegemea.
Watu wanaoendesha Injili ya Sayansi
MwanzilishiMwanzilishi & Mwenyekiti
Tiba ya Wanyama, Sayansi za Ubongo, Tiba Asili
Ni daktari wa wanyama toka Chuo Kikuu cha Sua, Morogoro. Muda wake mwingi zaidi amejikita katika kusoma, kufuatilia, na kutafiti sayansi za Ubongo, Biofizikia, na Historia za jamii za watu, na sayansi za watu 'Anthropolojia'. Ameandika Mjumuisho wa Vitabu 'Compendium' ya Ubongo wa Mtu mweusi yenye sehemu 5 'Volumes', ameandika Vitabu vingine vinavyohusu tiba ya mwili kupitia asili, Sayansi ya Uumbaji, Afrika haihitaji serikali, na Madhara ya Teknolojia na Vyakula vya kisasa'. Masomo yake pia hupatikana bure kupitia Blog za injili ya sayansi, vipindi vya Redioni, na Mitandao kadhaa ya kijamii. Kwa sasa ni Mwenyekiti wa Injili ya sayansi.
KatibuKatibu Mkuu
Elimu ya Sayansi, Fizikia na Kemia
Ni Mhitimu wa Shahada ya Sayansi na Elimu toka Chuo Kikuu cha UDISM DUCE, Tanzania. Mwalimu Wyclife ni Mdadisi na mwenye shauku Mahususi katika sayansi za Fizikia na Kemia. Wyclife anapenda kufundisha, kukuza mapenzi ya sayansi kwa wanafunzi, na pia kuandika vitabu vya afya na dini kama mwandishi na mwanzilishi wa Wiki eBooks Publishers. Kupitia msingi wake imara katika masomo ya sayansi, pamoja na Mapenzi yake makubwa katika Hekima za Vitabu vya Mithali, Zaburi, na Mhubiri, Amejitolea kuunda mazingira ya ujifunzaji yenye mvuto na ufanisi mkubwa, huku akiendelea kuboresha ujuzi wake na wa jamii yake kitaaluma. Yuko tayari kuchangia katika taasisi za elimu kama mwalimu mwenye motisha na anayejibadilisha kulingana na mazingira. Kwa sasa Mwl Wycliffe ni Katibu mkuu wa Injili ya Sayansi.
MhaziniMhazini
Afya ya Jamii, Bioteknolojia
Ni mtafiti wa kina na mwandishi anayependa uchunguzi wa maswali magumu ya kifalsafa ya maisha kupitia sayansi, akili, na tafakuri binafsi. Ni msomi wa Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Afya ya Jamii (Msc. Public Health Pest Management), na pia ana Shahada ya Kwanza (BSc) katika Bioteknolojia na Sayansi ya Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine, SUA, Morogoro Tanzania. Gamba amejikita sana kupambanua ufahamu wa kitaalamu na udadisi mkubwa kuhusu imani ya binadamu na uzoefu. Muda wote wa nje na kazi zake za kiofisi hupenda kuhariri vitabu na rasimu mbalimbali ili kusaidia watu wengine kudadavua hoja nzito kwa urahisi na uwazi zaidi. Kitabu chake cha A MAN WITH NO RELIGION ni safari yake ndefu ya kimawazo katika Kiini cha Imani, utambuzi binafsi, na kile kinachoitwa ukweli katika Ulimwengu wa uhalisia. Kwa sasa Gamba Manyama ni Mhazini wa Injili ya sayansi.
Injili ya sayansi inalenga kutengeneza kizazi ambacho kitakuwa na Elimu ya kujitegemea.
Injili ya sayansi imejikita kutoa masomo mbalimbali kivitendo kuhusiana na Elimu ya kweli na Malezi. Katika Kitengo cha Elimu na Malezi; Injili ya sayansi inashirikiana na wasomi mbalimbali wenye motisha ya kusaidia jamii zao kwa kutoa Elimu bora nje na mfumo tegemezi wa elimu. Malengo ya injili ya sayansi ni kutengeneza kizazi ambacho kitakuwa na Elimu ya kujitegemea.
Injili ya sayansi ina matawi yake ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali, huku Shule ya Sekondari ya Mzumbe, Morogoro, ikiwa Makao makuu kwa Shule zote. Tofauti na mfumo uliopo ambao waliojuu ndiyo wanapaswa kufikiria nini cha kuwafundisha waliochini, Injili ya sayansi inalenga waliochini kujua nini wanahitaji kufundishwa, kusoma, au kujisomea.
kuuliza maswali kuhusu kila aina ya imani, au misimamo iliyojengeka katika sayansi, falsafa, au mafundisho ya kidini kwa kutumia fikra huru na za msingi.
Kukuza hamu ya maarifa, na kuondoa hofu ya kukutana na hoja tofauti au za upinzani juu ya taarifa yoyote.
Tunategemea wanafunzi Kusoma kwa makini vitabu, kazi za kisayansi, maandiko ya kifalsafa, na dhana za kiteolojia zinazopendekezwa na Injili ya Sayansi.
ili Kujenga uwezo wa kimwili na kiakili wa kuhimili na kutawala mazingira katika nyanja za kisayansi, kijamii, kidini na kiuchumi.
na kuwa na uwezo wa kuzalisha mawazo mapya, Kujenga taswira, na kutengeneza mikakati ya kuendeleza maendeleo ya kisayansi ya Afrika.
Malengo makuu ya uongozi na kikundi yanayotuelekeza katika kutekeleza dira yetu.
Injili ya sayansi ukiachana na Uongozi wa juu, ambao unashikiliwa na Mwenyekiti, Katibu Mkuu, na Mhazini wake. Mfumo wake wa Uongozi umetawanyika 'Decentralized'.
Nguzo tatu zinazounga mkono maendeleo ya jamii kupitia Injili ya Sayansi.
Leadership & Education
Mafundisho ya vitendo kwa ajili ya elimu ya kweli nje ya mifumo tegemezi ya shule. Matawi ya wanafunzi katika shule mbalimbali yenye makao makuu katika Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro.
Science & Health
Huduma za afya zilizo kamili, ikijumuisha tiba ya kliniki, kinga, na mbinu za tiba asilia zinazoongozwa na wataalamu waliohitimu.
Agriculture & Environment
Uongozi wa kitaalamu juu ya afya ya mimea na wanyama, kilimo endelevu, na urejeshaji wa mazingira kwa maisha ya asili kama Bustani ya Eden.
Animal Health
Huduma za afya ya wanyama na elimu kuhusu matumizi sahihi ya protini za wanyama kwa ajili ya afya ya binadamu kupitia wataalam wa sayansi ya wanyama na madaktari wa mifugo.
Science & Technology
Mtazamo wenye uwiano kuhusu teknolojia kwa ushirikiano na wanafizikia na wahandisi wanaohamasisha maendeleo ya kiteknolojia kwa hekima huku wakitanguliza afya ya binadamu.
Theology & Philosophy
Uchambuzi sahihi wa kifalsafa na kiteolojia kupitia ushirikiano na wachungaji na wasomi wanaounga mkono tafsiri ya kibiblia na ukweli wa maadili.
Research & Publications
Maktaba pana ya vitabu, makala, na vifaa vya utafiti kutoka kwa waandishi wa ndani na nje kuhusu afya, sayansi, teolojia, na maendeleo ya binafsi.
Msaada wa kina kupitia elimu, ushauri, na programu za kijamii.
Jiunge na Injili ya Sayansi na upate fursa za kupata elimu, mtandao, na maendeleo.
Pata msaada wa moja kwa moja kupitia WhatsApp. Tuandikie ujumbe na tutakujibu haraka.
Wasiliana kupitia WhatsAppKukuza ujifunzaji na ukuaji wa akili kupitia ziara za kielimu na mijadala ya kitaaluma.
Tunapanga ziara za kielimu, ziara za kubadilishana maarifa, na mijadala ya kitaaluma iliyopangwa ili kukuza ujifunzaji na ukuaji wa akili miongoni mwa wanachama.
Ziara za timu na wajumbe
Uratibu wa matawi ya shule
Programu za kuwafikia jamii
WANDISHI wote wanaopendekezwa na Injili ya Sayansi. Vitabu hivi vina msaada mkubwa katika maarifa na maadili.
Uchambuzi wa kina juu ya sayansi, imani, na afya

Sayansi na Mazingira

Sayansi na Mazingira

Sayansi na Mazingira

Sayansi na Mazingira

Sayansi na Mazingira

Sayansi na Mazingira
Wasiliana nasi kwa kupata maelezo zaidi kuhusu shughuli zetu, vitabu, au kujiunga na Injili ya Sayansi.
Mahali
Sokoine University of Agriculture, Morogoro
Barua Pepe
info@injiliyasayansi.com
Simu
+255 628 231 767
Tuma Ujumbe
Tunashirikiana na shule, vyuo vikuu, makanisa, mashirika yasiyo ya kiserikali, na taasisi za kijamii kuandaa vipindi halali vya kujifunza na programu za kuwafikia watu.
Maarifa bila imani ni kama mti usio na mizizi — unakua lakini huna msingi.
Injili ya Sayansi